Mshambuliaji wa Leicester City ya nchini England, Jamie Vardy jana aliweka rekodi ya kipekee katika ligi kuu soka nchini humo baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester United, likiwa ni goli lake la 11 mfululizo msimu huu na kuivunja rekodi iliyowekwa na gwiji wa Manchester United, Ruud Van Nistelrooy aliyefunga katika michezo 10 mfululizo mwaka 2003.
Ruud Van Nistelrooy alikuwa mstari wa mbele kumpongeza nyota huyo raia wa uingereza kwa kulifuta jina lake na kisha kufungua ukurasa mpya huku akimtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka.
Mastaa waliocheza soka zamani ambao hivi sasa ni wachambuzi wa soka, wakiongozwa na Gary Lineker na Rio Ferdinand kupitia mitandao yao ya kijamii ya twitter na Facebook walimpongeza kijana huyo ambaye hadi sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao katika ligi hiyo.
Wachezaji wenzake wakiongozwa na mlinzi wa kulia wa Tottenham Hotspur, Kyle Walker wali-tweet pia kumpongeza mwenzao mara baada ya kufunga goli hill dhidi ya Manchester United.
Comments
Post a Comment