Mchezaji mkongwe wa zamani wa klabu za Juventus, Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane 'zizou' amemtaja mchezaji Eden Hazard wa Chelsea kuwa bora zaidi nyuma ya Ronaldo na Lionel Messi.
Zidane anasema alifurahia kuona Hazard anacheza katika kiwango cha juu kabisa msimu uliopita na kumtaka mchezaji huyo arudi katika kiwango chake baada ya kuhangaika msimu huu.
Real Madrid imekua ikihusishwa mara kadhaa sasa kutaka saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 24 na Zizou anaota hilo litokee haraka kwani anaamini Hazard ni kipaji kikubwa nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Kauli hii ya Zizou ni kutonesha kidonda kwa klabu ya Chelsea ambayo haiko sawa msimu huu na kwamba wanahitaji kuwatunza wachezaji wake bora kurudi katika kiwango chake cha msimu uliopita.
Comments
Post a Comment