HUYO NDO KINDA WA ARSENAL HARRY DONAVAN ALIYEJIUNGA NA MILLWALL



HUYO NDO KINDA WA ARSENAL HARRY DONAVAN ALIYEJIUNGA NA MILLWALL

KLABU ya soka ya Arsenal imethibitisha kuwa kinda wake, Harry Donovan, amejiunga na timu ya Millwall inayoshiriki Ligi daraja la kwanza England.

Donovan mwenye umri wa miaka 17, ni mmoja wa nyota waliokuwa wanachipukia kwenye kikosi cha Arsenal cha chini ya miaka 18 lakini klabu hiyo haikumpa mkataba wa soka la kulipwa pale kinda huyo alipotimiza miaka 17.

Kwa upande wake, kocha wa Millwall, Neil Harris alisema; "alikuja katika majaribio wiki iliyopita na kiukweli kafanya vizuri.

Atanufaika kuwa na sisi katika timu yetu, tutampa nafasi kubwa ya kuendeleza soka lake".


Comments