Moja ya kitu ambacho David Beckham ana kijutia katika maisha yake ya soka ni kushindwa kupata nafasi ya kurudi tena kukipiga Old Trafford tangu atupiwe virago na Sir Alex Ferguson mwezi January 2013 na kuuzwa Real Madrid.
David Beckham ambaye leo hii ataungana na kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson katika mechi ya kijamii ya kuchangia watoto Old Trafford, anaamini kuwa kuna kitu kinakosekana kwake tofauti na akina Scholes ama Giggs katika malegendari wa Manchester United.
Akimpa ushauri Cristiano Ronaldo kuhusu future yake amesema kuwa Ronaldo ni kipenzi cha mashabiki Old Trafford na pia ni mchezaji bora zaidi katika historia ya klabu na hivyo hakuna sehemu iliyo bora kwake kuichezea akaheshimika kama ataondoka Madrid zaidi ya Old Trafford.
Beckham ambaye pamoja na kucheza Real Madrid, LA Galaxy na baadae Paris Saint Germain anahisi alihitaji kurudi kucheza tena sehemu aliyokulia tangu akiwa mdogo, Manchester United.
Cristiano mwenyewe hajakanusha uwezekano wa yeye kujiunga pamoja na Wayne Rooney Old Trafford huku akisisitiza hivi karibuni kwamba anahitaji kumaliza mpira katika timu na ligi yenye ushindani mkubwa.
Comments
Post a Comment