HUU NDIO USHAURI WA BECKHAM KWA MEMPHIS DEPAY


HUU NDIO USHAURI WA BECKHAM KWA MEMPHIS DEPAY

Becks 1

David Beckham amemshauri winga wa sasa wa Manchester United mholanzi Memphis Depay kuwa asiiogope jezi namba 7 wala kuichukulia kwa mzaha na kwamba ni heshima kwake na kitu anachotakiwa kuona ni inspirational katika jitihada zake za kufikia mafanikio.

Memphis Depay ambaye huenda akacheza mchezo wa jumamosi dhidi ya Watford kama Anthony Martial atakua kaumia sana na timu ya taifa, itakua ni mara yake ya kwanza tangu alipotolewa muda wa mapumziko katika kichapo cha goli 3-0 toka kwa Arsenal mwezi September mwaka huu.

Lakini Beckham amemtaka winga huyo kutopata presha wala kuhisi majivuno kwa kupewa jezi huyo bali aone ni heshima na changamoto ya kujituma zaidi uwanjani.

Manchester United ilimsajili Depay kutokana PSV Eindhoven ya Uholanzi kwa ada ya pauni milioni 25 huku kocha Louis Van Gaal akimtaja Depay kama winga bora wa umri wake lakini ameshindwa kuonesha na sasa anatarajiwa kurudi tena uwanjani kama Martial atakua nje ya uwanja jumamosi hii na tutasubiri kuona nini anafanya.



Comments