Arsenal inakaribia kumalizana na mshambuliaji wake Alexis Sanchez juu ya mkataba mpya utakaomweka Emirates kwa miaka mitano zaidi.
Inaaminika nyota huyo wa kimataifa wa Chile tayari ameshakubali ofa ya mkataba mpya wa miaka mitano kwa mshahara wa pauni 155,000 kwa wiki.
Sanchez amebakiza miaka miwili na nusu kwenye mkataba wake wa sasa hivi unaomwingizia pauni 130,000 kwa wiki.
Arsenal inataka kuhakikisha mkali huyo haingii kwenye miaka yake miwili ya mwisho kabla hajasaini mkataba mpya.
Alexis Sanchez yuko mbioni kusaini mkataba mpya Arsenal
Sanchez anakaribia kusaini dili la £155,000 kwa wiki
Inaaminika mazungumzo ya dili jipya la Sanchez ndani Arsenal yamefika mahala pazuri
Comments
Post a Comment