Manchester city wanapanga kumfanya Pep Guardiola kuwa kocha anayelipwa pesa nyingi kuliko kocha yoyote duniani. Wamiliki wa Manchester city wana mipango ya kufanya makubwa na club yao baada ya kutumia pesa nyingi kujenga kikosi chao, sasa hivi wamehamia kwa upande wa kocha.
Mkataba wa Guardiola na Bayern Munich unaisha mwishoni mwa Summer ambapo kuna tetesi sana kwamba atasepa kwenye club hiyo na kujiunga na Manchester City ya EPL.
Kwa upande Man City wanapanga kumfanya Pep kuwa kocha anayelipwa pesa nyingi na kumpita Jose Mourihno ambae ndio yupo namba moja kwa sasa. Tetesi zinasema kwamba anaweza kulipwa zaidi ya £13.2million ambazo ndizo analipwa Jose Mourinho.
Habari inayosambaa kwa sasa ni kwamba ndani ya masaa 24 yaliyopita Pep Guardiola ameshafanya maamuzi ya kujiunga na Manchester city pale mkataba wake utakapoisha na kuwa kocha anaelipwa pesa nyingi zaidi.
Mchakato huu wa kutaka kumpata Guardiola kama kocha wa Manchester city umekua kimya kimya sana, pia Pep kama akihamia Manchester city anategemea kupata bonus pamoja na endorsement nyingine.
Comments
Post a Comment