Legendari wa Manchester United, Gary Neville amesema hadhani kama ni sahihi kwa klabu kuangalia yaliyopita zaidi ya kuangalia mbele. Neville anasema haungi mkono suala la Ronaldo kurudi tena Old Trafford na badala yake klabu ingekomaa kupata saini ya Gareth Bale.
Neville anasema inawezekana Ronaldo ni kipaji kikubwa kuwahi kucheza naye lakini Manchester United inahitaji kuzishinda hisia na kuangalia yajayo kwa kumsajili Bale na sio kumrudisha Ronaldo.
Akitoa sababu za kwanini haoni ni suala zuri, Neville anakumbusha jinsi mastaa wa zamani wa Newcastle United walivyoshindwa kuwika ujio wao wa Mara ya pili kikosini na hata kuishusha time daraja walipokua makocha.
Anasema kuna kipindi Liverpool nao walifanya, lakini hali ilikua ni mbaya na kwamba ni heri United wakaachana na mpango huo na kuangalia maisha mengine.
Ronaldo mwenyewe amekua akisisitiza kutaka kucheza na Wayne Rooney kwa Mara nyingine huku akisema amem-miss rafiki yake huyo wa zamani wa Old Trafford.
Comments
Post a Comment