Kama baba anapenda kutumia pesa basi lazima azitumie na kwa mwanae pia sio kwake tu. Hivyo hivyo amefanya Mayweather ambae ni maarufu sana kwa kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kujinunua magari ya kifahari.
Hivyo hivyo amemnunulia mwanae wa kiume Koraun zawadi ya birthday gari aina ya Mercedes C-Class Coupe ambalo thamani yake ni zaidi ya Tsh milioni 99. Mtoto huyo amefikisha miaka 16 na alivyokua na miaka 15 pia alinunuliwa gari aina ya Bentley maalum kwa ajili ya kuendesha kwenye mchezo wa golf.
Hivi sasa Mayweather ame-retire na anatumia muda wake mwingi kusafiri na kupumzika. Pia amekua karibu sana na rafiki yake Justin Bieber ambapo wamekua wakienda wote likizo na Mayweather akienda kwenye show zake.
Comments
Post a Comment