CRISTIANO RONALDO ATABIRIWA KUFUATA NYAZO ZA RYAN GIGGS



CRISTIANO RONALDO ATABIRIWA KUFUATA NYAZO ZA RYAN GIGGS

GWIJI wa Southampton Matt Le Tissier, amesema kuwa mkali wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anaweza kufuata nyayo za mchezaji mwenzake wa zamani, Ryna Giggs kwa kucheza miaka mingi.

Katika umri wa miaka 30, Ronaldo haonyeshi ishara yoyote ya kushuka kiwango baada ya kufunga mara mbili Los Blancos wakishinda 4-0 Ligi ya Mabingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk Jumatano usiku.

Giggs alitundika daluga zake Manchester United akiwa na umri wa miaka 40 mwaka 2014 na Le Tissier anahisi Mreno CR7 anaelekea katika nyendo hizo. 

"Ni mchezaji maridadi," aliiambia Sky Sport News "Haitanishangaza endapo ataendelea kucheza kama Ryan Giggs.

"Anajilinda na ana mtazamo sahihi, kama akiendelea na ari yake, nafikiri atadumu kwenye soka muda mrefu. Nadhani ana muda mwingi zaidi mbele yake wa kucheza soka zaidi."

Ronaldo ambaye aliondoka Man United na kutua Real Madrid mwaka 2009, anashikilia rekodi ya kuwa na magoli mengi katika klabu hiyo ya Hispania.


Comments