Lewandowski star wa Bundesliga ya Startimes amefanya vizuri sana kwenye mwanzo wa msimu huu kwa pande zote mbili kwa club na kitaifa.
Wakala wake Cezary Kucharski amesema kwamba Real Madrid wameshaonyesha nia ya kumsajili mchezaji wake. "Hauwezi kukataa kwamba club kama Real Madrid kuwa na intrest na mchezaji kama Lewandowski.", alisema wakala huyo.
Maneno haya yanafuatana yale ya awali ambapo club za EPL inasemekana nazo zinahitaji sana service ya Lewandoski na wameshafanya mawasiliano na wakala wake.
Kati ya club ambazo zinamuhitaji sana Lewandowski ni kama Chelsea ambao wanataka kutumia muda wa January kuimalisha kikosi chao na Real Madrid ambao wana tetesi za kutaka kuondokewa na mfungaji wao Ronaldo.
Comments
Post a Comment