CHICAGO BULLS YAINYOOSHA PACERS YENYE PAUL GEORGE ALIYE KATIKA KIWANGO BORA



CHICAGO BULLS YAINYOOSHA PACERS YENYE PAUL GEORGE ALIYE KATIKA KIWANGO BORA

BUTLER

Butler alifunga pointi 17 na alicheza kwa kuimarisha ulinzi mkali dhidi ya Paul  George katika umilki wa mwisho wa mpira wa Indiana Pacers. Hii ilipelekea  kuisaidia Chicago Bulls  kung'ang'ana na kuibuka na ushindi mgumu wa 96-95 dhidi  ya Pacers Jumatatu usiku.

" Jimmy alifanya baadhi ya michezo mizuri  kwa sisi ndani ya uwanja na kuchagiza ushindi, " kocha wa  Chicago Fred Hoiberg alisema.

"Siyo tu alichokifanya miwsho, lakini alifanya mengi makubwa na vikapu vya msingi alifunga." Butler alimbana Paul George aliyekuwa anajaribu kurusha mtupo wa ushindi, hivyo mtupo wake ukapea.

Huu ulikuwa ndo mtupo wa mwisho wa mchezo ambao Indiana Pacers walihitaji ili kujipatia ushindi, hivyo kupelekea vicheko kwenye benchi na mashabiki wa Chicago Bulls.

Ni mchezaji bora sana, moja ya guards ambao ni vigumu sana kuwakaba kikamilifu. Aliruka vyema, akajinyoosha, akaachia mpira lakini nikapata kuugusa na kusaidia kuokoa timu yangu, Jimmy Butler alisema juu ya Paul George.

Derrick Rose alikuwa na pointi 23 huku akipata mitupo  9 kati ya 18 aliyojaribu kwa Chicago , lakini alitoka huku zikiwa zimebaki takribani  dakika sita.

Ilibidi atoke baada ya  kuteguka na kutonesha eneo la  kifundo cha mguu wake wa kushoto. Doug McDermott alifunga pointi 11. Paul George alikuwa na pointi 26 kwa Indiana Pacers, na Monta Ellis alimaliza na pointi 20 .

CJ Miles alipata mitupo mitano  ya pointi 3 ikimsaidia kumaliza na  pointi 19.  Jordan Hill na Ian Mahinmi kila mmoja alinyakua rebounds 12.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

 


Comments