Mabao yaliyofungwa na Gary Cahill, Willian, Oscar na Kurt Zouma yameipa Chelsea pointi tatu muhimu kufuatia ushindi wake wa 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika mchezo wa kundi wa Ligi ya Mabingwa.
Wakati Chelsea ikiua 4-0, Porto iliyokuwa inaongoza kundi G, imeshushwa hadi nafasi ya pili baada ya kufungwa 2-0 na Dynamo Kyiv.
Porto na Chelsea zote zina pointi 10, lakini mabingwa hao wa England wanaogoza kundi G kwa wastani mzuri wa magoli.
Dynamo Kyiv ni tatu kwa pointi zake 8 na kufanya nafasi ya kufuzu kwenda 16 bora iwe wazi kwa timu zote tatu za juu kutegemea na matokeo yao ya mwisho yatakavyokuwa Disemba 9 ambapo Chelsea itaumana na Porto na huku Maccabi Tel Aviv wakiwa uso kwa uso na Dynamo Kyiv.
Msimamo wa kundi G huu hapa.
Comments
Post a Comment