Chelsea ya Jose Mourinho bado bado haiko sawa baada ya kuambulia pointi moja dhidi ya Tottenham kwenye mchezo wa Premier League.
Ni sare ambayo Tottenham itabidi wajialaumu kutokana na namna walivyodhibiti mchezo na kutengeneza nafasi za wazi ambazo kama wangezitumia vizuri basi wangeibuka na pointi tatu.
Mourinho ni kama vile bado anatafuta kikosi sahihi kwenye timu yake baada ya kumpiga benchi mshambuliaji namba moja wa timu hiyo Diego Costa.
Wakati wa mapumziko Costa alipasha mwili moto kama vile anatarajia kuingia uwanjani, lakini bado Mourinho akamsotesha benchi hadi mwisho wa mchezo.
Tottenham walicheza kama vile hawajawahi kupoteza mchezo wowote kwa namna walivyokuwa wakijiamini na kuziba mianya yote ambayo ingeweza kuwapa nafasi Chelsea ya kulijaribu lango lao.
TOTTENHAM XI (4-2-3-1): Lloris 6.5; Walker 6, Alderweireld 6.5, Vertonghen 6, Rose 7; Mason 6 (Lamela 55, 6.5), Dier 6.5, Dembele 6.5, Son 6.5 (Njie 73, 6); Eriksen 6.5; Kane 6.
CHELSEA XI (4-2-3-1): Begovic 6.5; Ivanovic 6, Zouma 7.5, Cahill 7, Azpilicueta 6; Fabregas 6.5, Matic 7; Willian 6 (Kennedy 88), Oscar 6.5, Pedro 6 (Loftus-Cheek - 91); Hazard 6.5.
Pedro (katikati) akikabiliana na Toby Alderweireld na kipa Hugo Lloris kwenye mchezo watani wa London
Pedro akisikitika shake likibabatiza mwamba
Harry Kane (katikati) alikuwa chini ya uangalizi mkali wa mabeki wa Chelsea
Son Heung-min (kushoto) akingalia mpira wake ukiokolewa na kipa wa Chelsea Asmir Begovic huku Branislav Ivanovic akiwa tayari kutoa msaada
Diego Costa (katikati) akiwa benchi
Costa akipasha mwili moto lakini bado akaendelea kusota benchi hadi mwisho wa mchezo uliofanyika White Hart Lane
Comments
Post a Comment