CHELSEA BADO HAIJAMKATIA TAMAA JOSE MOURINHO



CHELSEA BADO HAIJAMKATIA TAMAA JOSE MOURINHO
Jose Mourinho has endured a torrid season as Chelsea boss            with the champions sitting 16th in the table
UONGOZI wa klabu ya soka ya Chelsea umeanza kazi ya kutafakari jinsi gani utafanya ili timu hiyo iweze kufanya vizuri.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini Uingereza, imeeleza kuwa viongozi wa klabu hiyo wanajipanga upya.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuvuja habari kwamba huenda kocha Jose Mourinho atatimuliwa wakati wowote.

Tayari habari zaidi zimeeleza kuwa huenda klabu hiyo ikamchukua kocha mmojawapo kati ya Brendan Rodgers, Roberto Di Matteo na Guus Hiddink.
Hata hivyo Chelsea imesema bado ina imani na Mourinho na kwamba inajipanga upya kupitia yeye huku ikiamini kuwa kocha huyo bado ana uwezo wa kuirejesha klabu kwenye enzi za ushindi.
Chelsea inatarajiwa kufanya marekebisho kadhaa katika kikosi chake kwenye usajili wa dirisha dogo kabla ya kukifumua upya pale utakapowadia muda wa usajili wa majira ya kiangazi baada ya msimu huu kumalizika.


Comments