CARLO ANCELOTTI KUTUA LIGI KUU ENGLAND MSIMU UJAO


CARLO ANCELOTTI KUTUA LIGI KUU ENGLAND MSIMU UJAO

Carlo

Kocha muitaliano Carlo Ancelotti amesema anatamani kurudi tena kufundisha soka nchini England kwani anahitaji kufundisha katika ligi bora na yenye ushindani, lakini akasisitiza haitakua msimu huu bali msimu ujao wa 2015-16.

Ancelotti ambaye alitupiwa virago na boss Roman Abramovich wa Chelsea mwaka mmoja baada ya kuipa mataji mawili ya EPL na FA Cup klabu ya Chelsea, anatajwa kuja kurithi mikoba ya kocha Manuel Pellegrini wa Manchester City msimu ujao.

Carlo 1

Lakini Ancelotti anasisitiza kwamba anatamani kufundisha soka nchini England lakini asipopata timu atafundisha katika ligi nyingine kwani anasema alipata uzoefu mkubwa sana alipokuwa PSG (Ufaransa) na Real Madrid (Spain).

Akiongelea kuhusu Chelsea na yeye kuja kuchukua kiti cha Mourinho, King Carlo anasema klabu imefanya uamuzi sahihi kubakia na Mourinho kwani ni kocha bora na anajua vizuri tatizo lililopo Chelsea tofauti na meneja mwingine.

Carlo Ancelotti anaendelea na mapumziko take ya msimu mzima huko Vancouver, tangu atimuliwe na klabu ya Real Madrid msimu mmoja kabla ya kuipa kombe la kumi la klabu bingwa Ulaya 'La Decima'.



Comments