BENKI YA FIRST CAPITAL YASITISHA UDHAMINI LIGI YA GHANA


BENKI YA FIRST CAPITAL YASITISHA UDHAMINI LIGI YA GHANA

gfa-logoChama cha soka nchini Ghana(GFA) kimesema kuwa mdhamini wa Ligi ya Ghana (GPL) ambaye ni Benki inayofahamika kama First Capital Plus imesitisha mkataba wa udhamini wa Ligi ya Ghana kwa muda usiojulikana.

Udhamini wa Benki ya First Capital Plus una thamani dola milioni 10 kwa muda wa miaka 5.Kilichotokea mpaka mkataba huo ukasitishwa ni kuwa ripoti ya mwezi uliopita (Mwezi wa 10) toka katika taasisi hiyo ya kifedha ya First Capital inasema kuwa Utawala wa Benki haujaridhishwa na namna Ligi ya Ghana inavyoendeshwa.

Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa Benki ya First Capital haipati mrejesho mzuri wa uwekezaji waliofanya katika Ligi ya Ghana kutokana na uendeshaji usio na ufanisi wa Ligi hiyo.

Benki haitangazwi vya kutoshwa katika sehemu tofauti tofauti zaLigi hiyo kwa maana ya kwenye viwanja vya michezo,kwenye mikutano ya chama cha soka nchini Ghana nk.Kingine,mahudhurio ya viwanjani ni madogo hivyo chapa ya benki ya First Capital haifiki kwa watu wengi kama invyokusudiwa.

Sababu nyingine ni kubadilishwa mara kwa mara kwa ratiba ya Ligi ya Ghana kunaiumiza Benki hiyo katika matangazo yake lakini zaidi ni mwamko mdogo wa vyombo vya Habari katika kuitangaza Ligi ya Ghana.

nyantakyi 1Akizungumzia juu ya husitishaji wa mkataba huo, Rais wa Chama cha soka cha nchini Ghana Kwesi Nyantakyi anasema kuwa "kama chama cha soka wanaheshimu maamuzi ya Taasisi hiyo ya kifedha lakini wanaamini watakutana na viongozi wa benki ya Fisrt Capital kuangalia nini cha kufanya na kutatua changamoto zote zilizojitokeza.

Nyantakyi anaamini kuwa mabadiliko ya mfumo wa kiutawala wa benki hiyo ndiyo yamechangia kusitishwa kwa mkataba huo.Ila kamati ya utendaji ya Chama cha soka cha Ghana itakutana kujadili ripoti ya Bekni ya First Capital Plus na kutoa maamuzi.
Msimu wa Ligi Kuu ya Ghana unaanza mwezi ujao mwaka huu.



Comments