Barcelona imedhihirisha kuwa ipo kwenye kiwango cha kutisha baada ya kuichapa Real Sociedad 4-0 kwenye mchezo wa La Liga.
Aliyekuwa mwiba kwa Real Sociedad ni mshambuliaji Neymar aliyefunga mara mbili dakika ya 22 na 53 huku Lionel Messi na Luis Suarez kila mmoja akifunga mara moja.
Barcelona: Bravo; Alves (Adriano 62 mins), Pique, Mascherano, Mathieu (Alba 66); Rakitic, Busquets Iniesta; Messi, Suarez, Nemyar
Wafungaji: Neymar 22, 53, Suarez 41, Messi 91
Real Sociedad: Rulli; Elustondo, Gonzalez, Inigo Martinez, Izeta; Canales (Oyarzabal 58), Pardo, Granero, Prieto; Vela (Bruma 81), Agirretxe (Ortega 73)
Neymar akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza akiunganisha krosi ya Dani Alves dakika ya 22
Luis Suarez akiifungia Barcelona bao la pili
Neymar akishangilia na Suarez na Lionel Messi baada ya bao la tatu la Barcelona
Comments
Post a Comment