BABA WATOTO WA UWOYA APIGWA CHINI NA KLABU YAKE YA BONGO


BABA WATOTO WA UWOYA APIGWA CHINI NA KLABU YAKE YA BONGO

Ndikumana Hamad

Kikosi cha Stand United 'Chama la Wana' cha mjini Shinyanga kimemtema mchezaji wake Hamad Ndikumana kikidai umri wake ni mkubwa hivyo ameshindwa kuendana na kasi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Afisa habari wa Stand United Deokaji Makomba amesema, mwalimu Patrick Liewig ameamua kumuacha Ndikumana kwasababu ana umri mkubwa hivyo ameshindwa kuonesha kiwango kilichotarajiwa na timu hiyo wakati kikimsajili.

"Mwalimu alisema hatomtumia tena Ndikumana katika kikosi chake mara baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, sababu kubwa aliyoitoa mwalimu ni umri alionao Hamad Ndikumana na ameona itakuwa ngumu kumtumia tena kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara", amesema Makomba.

"Kwahiyo Ndikumana hatuponaye tena na tayari tumeshampa stahiki zake aangalie utaratibu mwingine kwenye vilabu vingine ambavyo zitamuhitaji ili aweze kuendelea na maisha yake ya soka".

Inadaiwa Ndikumana anaumri wa miaka 37 kitu ambacho kimepelekea ashindwe kutamba na kuwaongoza wachezaji vijana ambao hawana uzoefu mkubwa kwenye soka.

Ndikumana amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Star wa Bongo Movies Irene Uwoya na kufanikiwa kupata mtoto mmoja anayefahamika kwa jina la Krish.

Awali Ndikumana aliwahi kugoma kuondoka kambini kwa kile kilichodaiwa kutolipwa pesa zake za usajili. Mkali huyo wa Rwanda amedumu kwenye kikosi cha Stand United kwa muda wa miezi minne kabla ya kutemwa na Chama la Wana.



Comments