Baada ya urejeo wa Paul Kiongera, Simba SC inahitaji mmoja kati ya washambuaji hawa watatu.


Baada ya urejeo wa Paul Kiongera, Simba SC inahitaji mmoja kati ya washambuaji hawa watatu.

dfdffdf


Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Kiungo raia wa Kenya, Paul Kiongera anarejea katika klabu ya Simba SC, pia Mganda, Brian Majwega atasajiliwa wakati huu wa dirisha dogo la usajili ili kuongezea nguvu safu ya mashambulizi ambayo imeonekana kumtegemea mshambulizi mmoja tu kati ufungaji, Mganda, Hamis Kiiza ambaye ameshatupia kambani mara 8 katika mechi 5 alizoichezea timu yake msimu huu.

Ibrahim Ajib alifunga mara tatu kwa mpigo ' Hat-trick' katika game ya mwisho kabla ya ligi kusimama wakati Simba iliposhinda 6-1 dhidi ya Majimaji FC katika uwanja wa Taifa. Wachezaji watano tu kiujumla ndiyo wamefunga katika magoli 15 ambayo Simba wamefanikiwa kufunga katika mechi 9 za ligi kuu msimu huu.

Walinzi, Mohamed Hussein ' Tshabalala', Mzimbabwe, Justice Majabvi na Mganda, Juuko Murishid wamefunga goli moja moja kila mmoja. Ni wazi Simba ilihitaji usajili mpya lakini bahati mbaya licha ya kuwa na orodha ya wachezaji wa kutemwa, timu hiyo haijui kwanini ipaswa kufanya usajili mpya. Kitendo cha kurejea kwa Kiongera ni sawa na ' Kamari' kutoka na matatizo sugu ya goti ya kiungo huyo wa mashambulizi.

Akiwa "fiti', Paul ataongeza nguvu kubwa katika mashambulizi na bila shaka Kiiza atafunga zaidi na zaidi, lakini ' Kamari' siku zote huwa na matokeo ya aina mbili. Kupatia au kukosea kwa maana ya ' kuliwa au kula'. Kama ningepewa nafasi ya kuwashauri Simba wakati huu wa usajili, ningewaambia msaini mchezaji mmoja tu.

Pendekezo langu la kwanza ni Ame Ally, la pili ni Didier Kavumbagu, pendekezo la tatu ni Kelvin Ndayisenga. Timu inatafuta msaidizi mwenye uwezo wa kufunga kama Mganda, Kiiza na si aina ya mchezaji kama Majwega ambaye naweza kusema anakuja kufanya kile ambacho kinawezwa kufanywa na wachezaji kama Peter Mwalyanzi, Awadh Juma na Mwinyi Kazimoto.

Nguvu za Ame na uwezo wake wa kufunga unalingana na ule wa Kavumbagu, isitoshe ni wachezaji wenye uzoeufu zaidi. Labda iwe shida kuwapata kwa kuwa ni wachezaji wa Azam FC. Lakini kwa sasa wawili hawa ni wasugua benchi tu pale Azam FC. Simba wakienda kwa nguvu kama wanayotumia kuhakikisha wana msaini Majwega au kwa Mrundi, Laudit Mavugo.

Kwanini nimemtaka pia Kelvin Ndayisenga? Ni mfungaji ' bab kubwa' lakini si rahisi kuja Simba kwa sababu ya u-ghali wake. Kama ni ngumu kuwapata washambuliaji hao basi hakuna haja ya kusaini ni kuhakikisha Daniel Lyanga anakuwa huru na kuanza kuichezea timu hiyo.

Kama timu ina mastraika, Hamis Kiiza, Musa Mgosi, Ibrahim Ajib na Lyanga alafu haifungi basi kutakuwa na tatizo mahali-hasa kwa mwalimu. Inawezekana pia uwezo wa kocha mkuu Dylan Kerr ukawa chini. Kama sivyo mbona mabao ' ya kubahatisha'?



Comments