BAADA YA KUCHEZA KWA KUDUNGWA SINDANO ZA KUTULIZA MAUMIVU ...SERGIO RAMOS SASA KUKOSA MECHI NANE ZA REAL MADRID



BAADA YA KUCHEZA KWA KUDUNGWA SINDANO ZA KUTULIZA MAUMIVU ...SERGIO RAMOS SASA KUKOSA MECHI NANE ZA REAL MADRID

STAA wa timu ya Real Madrid, Sergio Ramos atalazimika kuzikosa mechi nane za timu hiyo kutokana na majeraha ya bega yanayomkabili.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, alijiumiza mwenyewe wakati wa mechi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk iliyopigwa Septemba mwaka huu na hadi sasa anaugua kwa muda wa miezi miwili.

Licha ya kuhitaji kupumzika, Ramos amekuwa akiendelea kucheza katika mechi muhimu za Real Madrid.

Miongoni mwa mechi alizocheza akiwa anatumia sindano za kutuliza maumivu, ni dhidi ya Paris Saint – Germain, Atletico Madrid, Celta, Vigo na Sevilla. 

Mechi nyingine ambayo nyota huyo alicheza akiwa amechomwa sindano ya kutuliza maumivu, ni ile ya Clasico dhidi yao na Barcelona iliyopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini kwa sasa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu ili kuuguza tatizo hilo.


Comments