Arsenal imefufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Champions League baada ya kuinyuka Dinamo Zagreb 3-0.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 6 na itahitaji kushinda mchezo wake wa mwisho Disemba 9 dhidi ya Olympiakos ili kusonga mbele.
Bayern Munich imejihakikishia kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuitandika Olympiakos 4-0.
Mabao ya Arsenal inayoshikilia nafasi ya tatu nyuma ya Bayern Munich na Olympiakos, yalifungwa na Mesut Ozil na Alexis Sanchez aliyetupia mipira wavuni mara mbili.
Kwa upande wa Bayern Munich wauaji walikuwa ni Douglas Costa, Robert Lewandowski, Thomas Muller na Kingsley Coman.
Huu ni msimamo wa kundi F huku kila timu ikiwa imebakiza mchezo mmoja.
Comments
Post a Comment