KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama kaanza kukata tamaa, staa wa Bayern Munich, Arjen Robben amesema kwamba anavyodhani tayari ameshaichezea timu yake ya taifa ya Uholanzi mashindano ya mwisho ya kimataifa.
Bada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka jana, Uholanzi pia imeshindwa kufuzu fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 baada ya kushika nafasi ya nne katika michuano ya kufuzu fainali hizo hatua ya makundi.
Kutokana na hali hiyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, anaamini kwa kushindwa namna hiyo, kunaweza kumkatisha tamaa mchezaji yeyote anayeichezea timu ya taifa.
"Kushindwa kufuzu fainali za Euro 2016, kumeathiri moyo wa kila mmoja wetu," Robben aliliambia jarida la Metro News.
"Pengine nimeshacheza mechi zangu za mwisho katika mashindano ya kimataifa," alisema nyota huyo.
Hata hivyo alisema kuwa pengine anaweza kufanya hivyo kama watafuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 kama atakuwa hajastaafu kucheza soka.
Comments
Post a Comment