ANDREY COUTINHO HABANDUKI YANGA



ANDREY COUTINHO HABANDUKI YANGA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, raia wa Brazil, Andrey Coutinho, alikuwa katika mchakato wa kukipiga barani Asia, lakini sasa atabaki Yanga, imefahamika.

Kwa mujibu wa habari za uhakika ambazo Saluti5 imezipata, Coutinho ambae hivi sasa yuko kwao Brazil kwa matatizo ya kifamilia, anatarajia kurejea nchini Jumamosi hii.

Mchezaji huyo aliyepata kuichezea klabu ya Rhukapura United ya Ligi Kuu Myanmar, aliwasiliana na klabu kadhaa za mataifa kadhaa ya Asia lakini wakala aliyekuwa akimuunganisha amesema dili imeshindikana ingawa hajafafanua.

Kutokana na maamuzi hayo, mchezaji huyo anapaswa kupigania namba kwenye kikosi cha Yanga ili kujitengenezea soko katika usajili ujao.

Imeelezwa kuwa Yanga ilikuwa ikivizia kumuuza mchezaji huyo na ingejaza nafasi yake kwa kusajili mchezaji wa kigeni.


Kutokana na kukwama huko, kocha Hans Van Der Pluijm atalazimika kufuta mpango wa kuongeza mchezaji wa kigeni kwa sasa.


Comments