Mchezaji wa kimataifa wa Togo mwenye miaka 31 amerudi tena uwanjani akiwa amevaa jezi Tottenham Hotspurs kucheza mechi ya kujitolea kwa ajili ya foundation yake ya SEA.
Kwenye hiyo mechi lengo kubwa ni kuchangisha pesa kutokana na viingilio ili kuchangia mfuko wa Sheyi Emmanuel Adebayor Foundation ambayo imeanzishwa na Adebayor na kusaidia mambo mbalimbali.
Nje ya kuandaa mechi hiyo kwa ajili ya uchangishaji wa pesa lakini pia Adebayor anatumia mechi hizi kwa ajili ya kujiweka tayari akisubili kujiunga na club mpya isiyojulikana baada ya kumalizana na Spurs.
Adebayor ameshindwa kucheza mechi za mwanzo wa msimu kutokana na muda wa usajili kupita na yeye akiwa bado kwenye mazungumzo na Spurs. Kiasi kikubwa anategemewa kupata club ya kuchezea ikifika mwezi wa kwanza kwenye dirisha dogo.
Comments
Post a Comment