ZAHA ASEMA ALISOTESHWA BENCHI MANCHESTER UNITED KWA KUPAKAZIWA KUTOKA KIMAPENZI NA BINTI WA DAVID MOYES
Wilfried Zaha mchezaji wa mwisho kusajiliwa na Sir Alex Ferguson, amesema miongoni mwa sababu ya kupigwa benchi na David Moyes ni shutuma zilizoibuliwa kuwa alitoka kimapenzi na binti wa kocha huyo aitwae Lauren.
Januari mwaka 2013 Ferguson alimsajili Zaha kwa pauni milioni 15 kutoka Crystal Palace lakini akamwacha kwa mkopo Palace hadi mwishoni mwa msimu.
Mrithi wa Ferguson, David Moyes hakuwa na la maana kwa Zaha zaidi ya kumpuuza na kumsotesha benchi kabla ya baadae mchezaji huyo kupelekwa kwa mkopo Cardiff City na baadae kuuzwa jumla kwa timu yake ya zamani Crystal Palace ambako kwa sasa anang'ara kupita maelezo.
Akizungumzia uvumi wa kutembea na binti wa Moyes, Zaha alisema: "Sikuwahi kutembea na binti wa Moyes, wala sikuwahi kuwa na tabia mbaya.
"Huo ni uvumi ulionitesa hadi nilipoondoka United, sikuwa na la kusema kwa wakati ule. Sikuwahi kuonana hata mara moja na Lauren na sijui ni wapi ulipotokea uvumi ule."
Zaha amefichua kuwa maisha yake ndani Manchester United hayakuwa na furaha
Katika muda wake aliokaa United, Zaha alipakaziwa kuwa ametembea na binti wa Moyes aitwae Lauren (pichani)
Zaha anasema hajawahi kukutana na Lauren na hajui tetesi zilitokea wapi
Zaha akiichezea United dhidi ya Wigan mwaka 2013 katika Community Shield
Zaha anadai hakuwa na uhusiano mzuri na boss wa zamani wa United David Moyes
Zaha hakuwa na amani ndani ya Manchester United
Zaha akimpita beki wa Manchester City Eliaquim Mangala (kushoto) wakati wa mchezo wa League Cup
Zaha akimiliki mpira mbele ya beki wa Leicester City Christian Fuchs kwenye uwanja wa King Power
Zaha sakifunga katika mechi ya 3-3 ya Premier League dhidi ya Newcastle ndani ya St James' Park msimu uliopita
Zaha akiwa na kocha wake Alan Pardew
Comments
Post a Comment