YOHAN CABAYE ASEMA ANTHONY MARTIAL WA MANCHESTER UNITED NDIYO HABARI YA 'MUJINI'



YOHAN CABAYE ASEMA ANTHONY MARTIAL WA MANCHESTER UNITED NDIYO HABARI YA 'MUJINI'

YOHAN CABAYE ana matumaini kuwa mshambuliaji mpya wa  Manchester United Anthony Martial (pichani juu) atang'ara kwa muda mrefu kwenye Premier League.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alisajiliwa kwa pauni milioni 36 kutoka Monaco  msimu huu huku ada yake ikitarajiwa kupanda hadi pauni milioni 58 kutokana na maendeleo yake yatakavyokuwa ndani ya Manchester United.
"Nina matumaini atakuwa supastaa katika Premier League"
Yohan Cabaye
Martial alifunga katika mchezo wake wa kwanza kwa Man United dhidi ya Liverpool na baada ya muda mfupi akawa ameshajikusanyia jumla ya mabao manne na kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba. 
Cabaye, nyota wa Ufaransa anayekipiga Crystal Palace  amesema hashangazwi na maendeleo ya haraka ya Martial  ndani ya Old Trafford.
Cabaye anasema: "Ni mchezaji kijana sana lakini kwa namna anavyocheza uwanjani na tabia yake ilivyo nje ya uwanja, anaoenekana kama mtu aliyepevuka. Ana uwezo wa kuhimili shinikizo  juu ya uhamisho wake wa bei mbaya.
"Nina matumani atakuwa supastaa katika Premier League, ni mechezaji mwenye kipaji cha hali ya juu."
Yohan Cabaye anayedai Anthony Martial atakuwa tishio



Comments