Mkongwe wa Barcelona Xavi Hernandez, anaamini kuwa Jack Wilshere ni moja kati ya wachezaji wa Arsenal na Uingereza wenye ubora wa hali ya juu sana pale tu anapokuwa fiti bila ya kusumbuliwa na majeraha yoyote.
Majeraha ya mara kwa mara yanayomkabili Wilshere yamekuwa yakimpa wakati mgumu sana kuwa katika kiwango bora kwenye misimu mingi, kiasi cha kushindwa kucheza hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi mwezi Agosti.
Lakini Xavi anasema kwamba Wilshere, ambaye aliposti picha kwenye Twitter akiwa na shati ya Arsenal yenye jina la 'Parlour 11' nyuma na nyingine ikiwa na jina la 'Bergkamp 10', ana uwezo mkubwa unamtofautisha na wachezaji wengi wa Kiingereza wa sasa huku akikumbushia kiwango kikubwa sana alichokionyesha dhidi ya Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2011.
'Alicheza mpira mkubwa sana dhidi yetu mwaka 2011,' Xavi alisema wakati akiongea na Sport magazine. Lakini bila ya kusahau alikuwa na umri wa miaka 20 au 21 (alikuwa ana miaka 19). Ni vibaya tu kuona ana majeraha ya mara kwa mara kwa miaka mingi mfululizo.
'Kama ataendelea kuwa kama alivyo atafanya makubwa sana katika klabu ya Arsenal ama timu ya taifa ya Uingereza. Ni mchezaji wa kipekee kabisa katika taifa la Uingereza.
'Hata kama amekuwa akitumia nguvu kwa kiasi fulani lakini ana kipaji cha aina yake, ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi na pia uwezo wa kumiliki mpira. Haonekani kama ni mchezaji wa Kiingereza!'
Comments
Post a Comment