XAVI AMESEMA KAMA ANGECHEZA EPL BASI ANGEJIUNGA NA HAPA


XAVI AMESEMA KAMA ANGECHEZA EPL BASI ANGEJIUNGA NA HAPA

gettyimages-114914934Xavi mchezaji mwenye historia na club ya Barcelona ameonyesha masikitiko yake kwa kutowa kucheza kwenye ligi ya EPL. Akiongea na EuroSport Xavi amesema, "Kuwa mkweli ni kwamba EPL ni ligi yenye mvuto sana kwa mchezaji yoyote, kuna viwanja vizuri, mashabiki jinsi wanavyo feel soka. Mambo ni mazuri kule".

Xavi akiendelea na interview hiyo aliongezea kuhusu club ambazo labda angeweza kujiunga nazo kama angepata nafasi ya kucheza kwenye EPL,"Kama ningepata nafasi ya kuchagua moja basi itakua club yenye historia kubwa kama Manchester united au Liverpool"

"Najua kuna club zimeibuka na kuwa kubwa na kuleta ushindani mkubwa mfano Manchester city, lakini kwangu mimi club kama Manchester united zinavutia kihistoria"



Comments