Manager Wenger hajakubali kabisa ishu ya kocha wa Liverpool kufukuzwa kazi kwenye club hiyo. Rodgers kutokana na matokeo mabaya ukilinganisha na uwekezaji uliofanyika ameshindwa kuonyesha uwezo wa timu yake kupata ushindi.
Wenger alisema ,"Tusisahau kwamba Liverpool haijakua bingwa kwa miaka mingi sana. Wameshinda mataji 18 tu kwenye championship. Walikuja karibu sana kushinda kwenye miaka 2 iliyopita kitu ambacho ni kizuri ukiangalia historia yao.Sasa sijui kwanini wamefanya haya maamuzi kwa sasa, ni vigumu sana kwangu mimi kuelewa."
"Nimeshangazwa sana na nimejiskia vibaya, nadhani unavyopoteza kazi ya maisha yako ni vigumu wakati mgumu sana na zaidi ya hapo ni ndani ya mechi 8 tu."
Comments
Post a Comment