WAYNE ROONEY, CARRICK NA ASHLEY YOUNG WALIVYOIUA MANCHESTER UNITED NDANI YA OLD TRAFFORD ...Middlesbrough yasonga mbele Capital One Cup
Manchester United iliyosheheni wachezaji wake wa kikosi cha kwanza, imeungana na vigogo wengine Arsenal na Chelsea kuiaga michuano ya Capital One Cup baada ya kunyukwa kwa penalti na Middlesbrough.
Mbaya zaidi ni kwamba United imeng'olewa mbele ya mashabiki 70,000 waliofurika kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford.
Kikosi cha United kinachanolewa na Louis van Gaal, kililazimishwa sare ya 0-0 katika dakika 120 na hivyo mchezo ukaamuliwa kwa mikwaju ya penalti ambapo wenyeji wakapoteza penalti tatu kupitia kwa wachezaji wake nyota Wayne Rooney, Michael Carrick na Ashley Young.
Kiujumla Middlesbrough ilicheza vizuri zaidi na kustahili kusonga mbele licha ya madai ya United kulalamikia kunyimwa penalti baada ya mpira Daniel Ayala kuunawa mpira ulipigwa na Anthony Martial.
MANCHESTER UNITED (4-3-3): Romero 6.5; Darmian 6, Smalling 6, Blind 5.5, Rojo 6.5 (Young 61 6); Carrick 6, Fellaini 6, Pereira 5.5; Lingard 6, Wilson 5.5 (Rooney 45 6), Depay 5.5 (Martial 70 6)
MIDDLESBROUGH (4-2-3-1): Mejias 7; Kalas 7, Ayala 7.5, Gibson 6.5, Friend 6.5; Stephens 6 (Clayton 114), Leadbitter 6; Nsue 6, Downing 6.5, de Pena 6 (Zuculini 79); Kike 6 (Nugent 84)
Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney akipiga penalti iliyookolewa na kipa wa Middlesbrough Tomas Mejias
Stewart Downing wa Middlesbrough (wanne kushoto) akisalimia mashabiki baada ya Rooney kukosa penalti kwa upande wa United kwenye dimba la Old Trafford
Michael Carrick akigonga mwamba na kuikosesha United penalti
Ashley Young akikosa penalti ya tatu kwa upande wa United
Middlesbrough wakishangilia ndani ya Old Trafford
Ben Gibson na wachezaji wenzake wa Middlesbrough wakishangilia baada ya kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya Capital One kwa kuing'oa Manchester United
Wachezaji wa Manchester United wanavyoonekana baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya Capital One Cup Jumatano usiku
Kocha wa United Louis van Gaal akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs kwenye mchezo wa Capital One
Comments
Post a Comment