WANASOKA WATANO MAARUFU DUNIANI WALIOSTAAFU SOKA KISA POMBE



WANASOKA WATANO MAARUFU DUNIANI WALIOSTAAFU SOKA KISA POMBE
Walevi
5. George Best
Best
Mchezaji huyu wa zamani wa Manchester United ni starmkubwa ambaye hahitaji utambulisho mkubwa kutokana na kile alichokifanya akiwa na klabu ya Mashetani Wekundu. Ameshinda Kolbe la Ulaya (kwa sasa Ligi ya Mabingwa Ulaya) mwaka 1968. Alikuwa mahiri sana mbele ya goli lakini pia alikuwa mahiri wa kufunga kwenye baa na wanawake pia.
Ikafikia wakati akalazimika kupandikizwa ini jipya mwaka 2002 lakini alikufa mnamo mwaka 2005. Alifunga mabao 181 katika michezo 474 akiwa na klabu ya Manchester United.
 
4. Paul Gascoigne
Gascoigne pia najulikana kwa jina la Gazza, lilikuwa ni jina alilopewa kutokana na kuhudumu katika nyumba ya soka ya kiingereza katikati ya miaka ya 80 na 90. Alikuwa ni kijana mwenye kipaji lakini kupenda pombe na madawa na kucheza kamari  kupindukia kulimaliza tasnia yake mapema kabisa. Bado yuko hai mpaka sasa lakini ni aibu kubwa sana kwa mwanandinga huyo wa zamani kutokuwa na fursa hata ya kutoa ujuzi wake kwa vijana waliopo sasa kutokana na ulevi wake wa kupindukia.
Alizichezea klabu za Everton, Tottenham Hotspur na nyinginezo ambapo aliweza kupachika mabao 110 katika michezo 468 aliyocheza.
 
3. Tony Adams
Huyu ni nguli wa Arsenal, ambaye sanamu yake iliyopo klabuni hapo inaeleza kila kitu kuhusu yeye. Nguli huyu ni mlevi kupindukia ambaye aliuanza ulevi huo tangu miaka ya 1980. Amecheza michezo 504 ndani ya klabu ya Arsenal akifunga mabao 32. Alikuwa ni mtu mpambanaji maarufu sana wa klabu ya Arsenal kwenye kipindi chote ambacho aliitumikia klabu hiyo, lakini tabia yake ya ulevi ilimaliza soka lake vibaya.
Hata hivyo, Adams aliacha rasmi kunywa pombe manmo mwaka 1996 na kuandika kitabu chake ambacho kilivunja rekodi ya mauzo. Baadaye alianzisha programu maalum kwa ajili ya kusaidia vijana kuachana na tatizo la ulevi wa kupindukia.
 
2. Andriano
Huyu ni staa mwingine wa Brazil ambaye kipaji cha soka kiliharibiwa na pombe na wanawake. Kutoka kukipiga kunako klabu ya Inter Milan mapaka AS Roma, alikuwa ni moja ya wachezaji 'mbavu' mwa kipindi fulani katika ulimwengu wa soka.
Alipachika mabao 176 katika michezo 394 katika vilabu vyote alivyochezea huku pia akifunga mabao 27 katika michezo 48 kwa taifa lake la Brazil. 
Aliharibu kabisa kipaji chake kutokana na kuendekeza pombe kupitiliza. Ilifika wakati alikuwa hata hahudhurii mazoezini na kuendekeza kujirusha katika kumbi za starehe. Pengine angeweza kufikia mafanikio ya akina Ronaldo kama angeweza kujiweka mbali na suala la starehe na ulevi wa kupindukia na wanawake.
 
1. Diego Maradona
Sote kwa pamoja tunamjua Maradona kwa sababu ya mafanikio yake makubwa katika mchezo wa soka na ulevi wake wa Kokeni ambao ulimdondosha rasmi katika soka. Kitu ambacho watu wengi hawafahamu ni kwamba, huyu ni nguli wa Argentina ambaye alishinda kombe la dunia akiwa ni mlevi wa kupindukia. 
Katika kitabu alichoandika baada ya kustaafu soka kinachojulikana kwa jina la 'Hand of God' , alikiri kuwa mara zote alikuwa akinywa whiskey kila siku usiku. Pengine angetulia angeweza kufunga zaidi ya magoli 346 katika maisha yake ya soka.


Comments