WACHEZAJI WANAOMCHUKIA ZAIDI VAN GAAL KWENYE MAISHA YA SOKA



WACHEZAJI WANAOMCHUKIA ZAIDI VAN GAAL KWENYE MAISHA YA SOKA
Ribery-Van-Gaal
9. Hristo Stoichkov: Mchezaji wa zamani wa Barcelona 
"Van Gaal huwafanya wachezaji wateseke, ukiangalia yeye mwenyewe alikuwa mchezaji wa kawaida sana," alisema mchezaji huyo wa zamani wa Bulgaria. "Anaharibu wachezaji wote, kwa sababu ni mtu wa kawaida, angalia vizuri wachezaji ambao wameondoka kwa sababu yake. Kwanza kabisa aliiharibu Barcelona kwa kipindi hicho, na ikachukua muda mrefu mno kuijenga upya."
 
8. Rivaldo: Mchezaji wa zamani wa Barcelona
"Van Gaal ni sababu kubwa ya kuondoka kwangu. Simpendi kabisa van Gaal, na nina uhakika kwamba hanipendi pia," alisema Rivaldo. 
7. Giovanni: Mchezaji wa zamani wa Barcelona.
"Van Gaal ni Hitler wa wachezaji wa Kibrazil," alisema Giovanni. "Ana majivuno, anaringa sana yaani, kifupi ana matatizo sana. Maisha kati yangu na yeye yalikuwa ni magumu na mabaya sana, Wabrazil hawamtaki kabisa, amenifanya nishuke kiwango lakini vilevile aligombana na Rivaldo pamoja na Sonny Anderson.
"Mara zote alikuwa akituambia hatukuwa tukifuata maelekezo yake vizuri mazoezini. Najua inawezekana hana mawazo ya kisoka, hajui chochote, kwa kipindi chote nilichokuwa naye nilikuwa nikifanya mazoezi ya aina moja tu, ni kama mgonjwa ama chizi vile."
 
6. Lucio: Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich
"Ni ukweli usiofichika kwamba kila kocha ana falsafa zake. Lakini hata hivyo, Van Gaal kwa kifupi hakuwa na heshima kwangu. Nilistahili kuwa na heshima zaidi ya aliyokuwa akinipa."
 
"Van Gaal alinipa maumivu zaidi ya mtu yeyote katika ulimwengu wa soka. Hakuwa hata akiongea nami kabla ya baadaye kusema kwamba sikuwa nahitajika tena klabuni pale. Inahuzunisha sana kwa kweli. Nilikuwa na wakati mzuri sana pale Bayern na tulishinda makombe ya kutosha tu. Haikuishia hapo tu. Nilishinda kombe la Shirikisho mara mbili, kombe la dunia nikiwa na Brazil na kutangazwa kuwa beki bora wa ligi ya Bundesliga. Mimi sio kijana ambaye natakiwa kuthibitisha thamani yangu kwa kocha mpya."
 
5. Rafael Da Silva: Mchezaji wa zamani wa Manchester United.
"Najua hakuwa akinipenda, inawezekana sababu ni mimi kuwa Mbrazil, labda kweli ila sina uhakika na hilo.
"Najua historia yake kuwa huwa hapendi wachezaji wa Kibrazil, lakini siwezi kusema'Oh, hapendi Wabrazil'
"Kiukweli sijui kwa sababu tangu Anderson aondoke, nilibaki mimi pekee ambaye ndiye nilikuwa Mrazil."
4. Angel Di Maria: Mchezaji wa zamani wa Manchester United.
"Van Gaal ana falsafa zake na moja ya vitu vilivyonifanya mimi kuondoka ni kwamba,"Di Maria alisema. "Ni vigumu mno kuendana na Van Gaal. Nilikuwa na migongano mingi sana na yeye.
 
"Nilianza vizuri sana pale Manchester United lakini pale tu milipopata majeraha, mambo yakaanza kwenda mrama na ndipo Van Gaal alipoanza kunichezesha nafasi tofauti. Na nilipozungumza na (Laurent) Blanc akaniambia kuwa angenichezesha katika nafasi ile ile niliyokuwa nikicheza Madrid endapo nitajiunga na PSG."
 
3. Luca Toni: Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich.
"Kifupi ni kwamba Van Gaal hakutaka kufanya kazi na mimi, anawafanya wachezaji kama vitu visivyobadilika," alisema Toni. "Kocha alituhakikishia kuwa anaweza kumwacha mchezaji yeyote. Aliamua kufanya kwa vitendo lakini kwa njia ya kifasihi kwa kuvua suruali yake. Sikuwahi kukutana na kitu kama hicho, yaani ilkuwa ni kitu cha ajabu kabisa. Lakini bahati nzuri sikuwa nimeona chochote, kwa sababu sikuwa mstari wa mbele kama wenzanu wengine."
 
2. Frank Ribery: Mchezaji wa Bayern Munich
1. Zlatan Ibrahimovic: Mchezaji wa zamani Ajax Amsterdam.
'Alikuwa ni kama dikteta.'


Comments