Brendan Rodger ameachishwa kazi na club yake ya Liverpool na hivi sasa kocha anategemewa sana kuchukua hiyo mikoba ni Klopp. Sasa kwasababu hana power tena kwenye club, wachezaji wakua huru kuzungumza mambo ambayo yalikua moyoni wakati wa utawala wa Rodgers. Mmoja wapo ni Sakho ambae ame-signed mkataba mpya na Liverpool ametoa ya moyoni.
Sakho anasema alivyokua chini ya Brendan Rodger ilikua hivi,"Tuseme kipindi cha kifupi ambacho nilikua sichezi nilikua kama simba mtoto ambaye nimefunigiwa ndani ya chumba wala sipewi msosi. Sasa ukinifungulia geti sasa hivi lazima nionyesha njaa yangu".
Pia alimsifia captain wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard kwamba ni mfano mzuri sana kwa wacheza soka. "Mara nyingi Gerrard ananitumia meseji ndogo kuniambia kwamba nacheza vizuri na pia anajivunia mimi mfano kwenye mechi ya Bordeaux nilivyopewa kitambaa cha u-captain"
Comments
Post a Comment