TOTO AFRICAN WATAKIWA KUSHIKAMANA VINGINEVYO ITAKULA KWAO


TOTO AFRICAN WATAKIWA KUSHIKAMANA VINGINEVYO ITAKULA KWAO

VIONGOZI wapya wa klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza wametakiwa kujenga umoja ili kuiwezesha timu yao kufanya vema katika Ligi kuu Tanzania Bara na kupiga hatua kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi TFF, mwanasheria Aloyce Komba, mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi.
Toto Africans iliyokuwa katika malumbano ya kiuongozi kwa muda mrefu, hatimaye wiki iliyopita ilifanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti na Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.
Waliochaguliwa katika uchaguzi wa Klabu hiyo yenye makao makuu yake Mtaa Kishamapanda, ni Godwin Aiko kuwa Mwenyekiti mpya wa Klabu, wakati Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lushinge Lushinge na Timoth Kilumule.
"ninawaomba Viongozi mliochaguliwa mshirikiane na wenzenu waliopo kuiletea Toto mafanikio ya kisona na kiuchumi, mkishirikiana naamini mnaweza kuwavutia wanachama wengi na mashabiki wa kuisapoti Klabu yenu," alisema Komba.
Kufuatia uchaguzi huo, salamu za pongezi kwa viongozi wapya na Klabu kwa ujumla, zinazidi kumiminika kutoka kila pande ya nchi.


Comments