MKONGWE wa kike wa sanaa ya filamu, Suzan Lewis 'Natasha' ametamba kuwa, kujiheshimu kwake na kujiweka mbali na maskendo ni kati ya sababu zinazomfanya aendelee kuwa juu katika filamu hapa Bongo.
Akizungumza na Saluti5 nyumbani kwake Yombo, jijini Dar es Salaam, Natasha alisema kuwa amejitahidi kuwa mwigizaji anayepaswa kutolewa mfano kwa kujiepusha na yale yote yanayoweza kumshushia heshima.
"Wacheza filamu wengi hapa nchini wamekuwa ni wanaopanda na kushuka ama kupotea kabisa kwenye gemu, kutokana na kuingia kwa kishindo na hatimaye kujiingiza kwenye kashfa mbalimbali wakidhani ndio wanatengeneza majina yao," alisema Natasha.
Natasha alisema kuwa, siku zote jina la msanii kwenye muvi hutengenezwa na namna yeye mwenyewe anavyojiweka kwa kuigiza vizuri pamoja na kutunza heshima yake mbele ya jamii inayomzunguuka.
Comments
Post a Comment