STARS YASONGA MBELE LICHA YA KUPOTEZA MALAWI


STARS YASONGA MBELE LICHA YA KUPOTEZA MALAWI

Kikosi cha Stars kilichoanza leo dhidi ya UgandaPamoja na kufungwa bao 1-0 na Malawi, timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeafanikiwa kufuzu raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kombe la dunia, mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa Kamuzubanda, Blantyre nchini Malawi.

Katika mchezo huo ambao uliojawa hisia ya aina yake wenyeji Malawi walijipatia goli lao kunako dakika ya 42 ya mchezo likiwekwa kimiani na John Banda ambaye aliupiga kwa umahiri mkubwa mpira wa kuzungusha na kumgonga beki wa Stars na kutinga moja kwa moja wavuni mwa Stars na kumwacha Ali Mustafa akiruka bila ya mafanikio.

Hata hivyo, pamoja na matokeo hayo, Taifa Stars imefanikiwa kusonga mbele baada ya ushindi walioupita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wa mabao 2-0.

Stars inapita kwa jumla ya mabao 2-1 na inatarajiwa kukutana na miamba ya soka ya kaskazini mwa bara la Afrika, Algeria.



Comments