STAR WA SERIE A AMFUKUZA KAZI AGENT WAKE WA MIAKA 10 NA KUMPA KAZI MKE WAKE


STAR WA SERIE A AMFUKUZA KAZI AGENT WAKE WA MIAKA 10 NA KUMPA KAZI MKE WAKE

2D1FEF5B00000578-0-image-a-14_1444082364529

Mchezaji wa Inter Milan Mauro Icardi amemuachisha kazi agent wake ambaye alikua anafanya nae kazi kwa muda wa miaka 10 Abian Moreno na kumpa kazi mke wake.

Striker huyu ambae ana miaka 22, tangu akiwa ana miaka 12 alikua ana wakilishwa na mfanyabiashara Moreno lakini hivi karibuni wakala huyo alitoa siri kwamba ameachishwa kazi.

Wakala Moreno alisema kwamba mchezaji huyu Mauro Icardi alikua ana uhusiano wa karibu sana na mchezaji mwenzake Maxi Lopez ambae alikua mume wa Nara zamani. Baadae akamchukua tena huyo huyo mwanamke wa rafiki yake na kumuona mbele ya ndugu zake 12. Hivi sasa amefanya kuwa wakala wake.

Ukichana na haya maisha binafsi ya wachezaji wa Serie A unaweza kufuatilia maisha yao ya uwanjani wakiwa na club zao mbalimbali. Mechi za Serie A zinaonekana kupitia StarTimes.



Comments