Sir Alex Ferguson amekiri kuwa Ryan Giggs angeweza kuwa mrithi wake kama angestaafu kusakata kabumbu wakati akiwa na umri wa miaka 35.
Giggs ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Louis van Gaal, alitundika daluga akiwa na umri wa miaka 40 huku mchezo wake wa mwisho ukiwa ni dhidi ya Hull City mwezi Mei mwaka 2014.
Ferguson amesema: "Kama Ryan Giggs angestaafu miaka sita au saba iliyopita, basi huenda muda angekuwa kocha mkuu wa Manchester United.
"Hakuna ubishi, kama angestaafu akiwa na umri wa miaka 35, ningemfanya msaidizi wangu na hiyo ingempa nafasi ya kuchukua moja kwa moja nafasi yangu pale nilipostaafu.
"Angepata uzoefu mkubwa chini yangu kama anaoupata kwa Luis van Gaal hivi sasa. Hata hivyo sikuwahi kumwomba atundike daluga."
Ryan Giggs (kulia) kwa sasa ni kocha msaidizi Manchester United chini ya Louis van Gaal (kushoto)
Sir Alex Ferguson amekiri kuwa Giggs angeweza kuwa mrithi wake
Comments
Post a Comment