SIR ALEX FERGUSON AMHURUMIA VAN GAAL



SIR ALEX FERGUSON AMHURUMIA VAN GAAL

KOCHA mstaafu wa Manchester united, sir Alex Ferguson amesema anamhurumia kocha wa sasa wa klabu hiyo, Louis Van Gaal.
Sir Ferguson alifichua siri ya kwanini United imekosa mafanikio tangu alipoondoka yeye na kusema, anajua hata Van Gaal atateseka kama mtangulizi wake, David Moyes.
"Siri ya kuvurunda kwa United ni kukosa mchezaji mwenye kipaji binafsi anayeweza kuisaidia timu, mfano wa alivyokuwa Dwight Yorke," alisema.
Alimfagilia mshambuliaji huyo raia wa Trinidad and Tobago akisema alionyesha uwezo tangu siku ya kwanza kutua Old Trafford.
"United haijapata washambuliaji wenye uwezo wa kuamua matokeo, alipotua Yorke tulimpatia pacha wa uchezaji, Andy Cole na wawili hao ndio waliofanya United ifufuke baada ya kumalizika kwa zama za Eric Cantona," alisema.
Alisema, Yorke alifanya kile walichokitaka ambacho ni kufunga na uhamisho wake kutoka Aston Villa ukawa wa mafanikio na aliwabeba hadi siku anaondoka.


Comments