SIR ALEX FERGUSON AMESEMA HIVI KUHUSU JURGEN KLOPP



SIR ALEX FERGUSON AMESEMA HIVI KUHUSU JURGEN KLOPP

ferg

Kila mtu anatoa maoni yake kuhusu uteuzi mpya wa kocha wa Liverpool, lakini maoni ya watu wenye uzoefu na EPL yanatakiwa kuzingatiwa zaidi.

Sir Alex pia amehusika kwenye maoni juu ya Klopp kujiunga na Liverpool, Fergie amesema hivi ,"Ni uteuzi mzuri, namjua vizuri kupitia kwenye mikutano yetu ya darasa la ukocha tukiwa Geneva. Klopp ni mtu makini na pia anapenda kujua kila kitu na kujaribu kukitumia kwenye kazi. Pia anajua nini anakitaka akiwa na mipango yake kama tulivyoona alivyofanya vizuri na Dortmund. Nadhani atafanya vizuri, sitaki kusema hivyo kwasababu ni Liverpool lakini bila shaka lazima atafanya vizuri"

Pia fergie ameongezea kitu kimoja kwamba ni vizuri kama Klopp akifanya kazi mwenyewe bila kuingiliwa na wamiliki, "Kama haumuamini manager wako sasa utamuamini nani? Huyu ndio mtu pekee anatakiwa kusema mchezaji anamtaka na akacheze wapi. Kuna haya mambo ya kibiashara sana kwenye soka, nadhani kuna wakati yanakosewa. Kama haumuamini kocha kwanini umempa kazi. Sidhani Klopp aalikubali hili swala"



Comments