Nchini Italia michezo ya ligi hiyo (Serie A) itaendelea katika viwanja mbalimbali, kubwa nchini humo ni uchunguzi wa polisi juu ya uuzwaji wa matangazo ya television ya Serie A.
Waendesha mashtaka wa polisi wanasema kuwa, kulikuwa na harufu ya rushwa katika ugawaji wa 'tenda' za Serie A na kutofuatwa kwa kanuni za manunuzi.
Kampuni ya Media Set inayomilikiwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Italia na pia mmiliki wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi ni miongoni mwa makampuni yaliyopewa haki za matangazo ya television.
Jeshi la polisi tayari limeshaanza uchunguzi juu ya kampuni hiyo. Kampuni nyingine iliyopewa tenda ya kuonesha ligi ya Serie A ni pamoja na Sky Italia, katika uchunguzi huo binamu wa Rais wa FIFA Sepp Blatters anayefahamika kwa jina la Felipe Blatter naye anachunguzwa kupitia kampuni yake ya uwakalawa kuuza matangazo ya television inayofahamika kama In front Sports and Media.
Ikumbukwe kuwa Serie A itakuwa na mechi kubwa mbili siku ya Jumapili za Fiorentina dhidi ya Napoli na Inter Milan dhidi ya Juventus mchezo uliobatizwa jina la 'Derby De Italia'.
Comments
Post a Comment