Manchester City inahofia kumkosa mshambuliaji wake tegemeo Sergio Aguero katika mchezo dhidi ya wapinzani wapo Manchester United baada ya nyota huyo kuumia akiwa na timu ya taifa.
Timu hizo zinakutana wiki mbili zijazo katika mchezo wa Premier League lakini sasa Aguero yuko mashakani baada ya kupata maumivu ya msuli wa paja.
Sergio Aguero mwenye umri wa miaka 27, aliondolewa uwanjani na machela Alhamisi usiku katika mchezo wa Argetnina na Ecuador.
Aguero bado hajawasili Manchester lakini tayari Man City wanahofia kuwa watamkosa mkali huyo katika mechi zao kadhaa.
Sergio Aguero akitoloewa nje kwa machela
Aguero sasa hatarini kuikosa Manchester United
Comments
Post a Comment