Kiungo wa zamani wa Manchester United na England, Paul Scholes amemtetea nahodha wa Manchester United Wayne Rooney na kudai kuwa ni vigumu kwa straika yeyote yule kufunga kwa mfumo na staili ya Van Gaal.
Paul Scholes amesema amecheza na washambuliaji nguli duniani wakiwemo Rud Van Nisterlooy, Yorke na Teddy Sheringham lakini akasisitiza kuwa mfumo anaoutumia Van Gaal ungewapa wakati mgumu washambuliaji hao kufumania nyavu.
Anasema United hii ya Van Gaal, ndio timu ambayo asingetamani kuichezea kutokana na kutokua na mipango ya ushindi huku akilalamikia suala la kumiliki mpira kwa muda mrefu bila mipango ya kulisakama lango la timu pinzani. Anaendelea kusema kuwa United inahitaji ku-risk zaidi na kwenda mbele kuongeza presha.
Akiungwa mkono na kiungo mwenza wa zamani Nick But amesema Rooney ndio tegemeo la timu hivi sasa na kwamba ameishaibeba timu hii kwa miaka mingi hivi sasa na kwamba kama nahodha bado amekua akitimiza majukumu yake vizuri na kuiweka timu mabegani.
Comments
Post a Comment