Sam Allardyce ameonekana ni mwenye ari na furaha tayari kwa kuanza kibarua kipya cha kuinoa Sunderland inayosuasua kwenye Ligi Kuu ya England.
Kocha huyo wa zamani wa Newcastle alionekana hivyo pale alipotua kwenye uwanja wa ndege wa Manchester ikiwa ni mwanzo wa mtihani wake uliomshinda kocha Dick Advocaat aliyebwaga manyanga baada ya mwenendo mbaya wa timu.
Sam Allardyce mwenye umri wa miaka 60, amesaini mkataba wa miaka miwili kuikochi Sunderland.
Sam Allardyce akiwa uso kwa uso na kamera za waandishi wa habari maara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Manchester
Comments
Post a Comment