ROONEY AWEKA REKODI, AWAPOTEZEA WANAOMKEJELI


ROONEY AWEKA REKODI, AWAPOTEZEA WANAOMKEJELI

Wayne Rooney vs EvertonNahodha wa United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney jana alifunga goli katika ushindi wa mabao 3-0 nyumbani kwa Everton timu yake ya zamani, na kuweka rekodi ya kufikia magoli 187 aliyonayo Andy Cole nyuma ya Alan Shearer mwenye magoli 260 katika chati ya ufungaji bora wa muda wote wa ligi kuu England.

Rooney pia aliifunga klabu yake hiyo ya zamani tangu alipofanya hivyo mara ya mwisho 2007 katika uwanja wa Goodson Park.

Baada ya mechi hiyo Rooney ambaye amekua akipitia kipindi kigumu tangu kuanza kwa msimu huu, alipoulizwa kuhusiana na wanaomsema kuwa hawezi kufunga, Wazza alisema, "nimezoea. Imekua ni kawaida katika maisha yangu yote ya soka. Muhimu kwangu ni nini meneja na wachezaji wenzangu wanafikiri kuhusu mimi".

Kocha wake Louis Van Gaal hakusita kuonesha furaha yake kwa nahodha wake huyo huku akiwaambia waandishi wa habari kuwa siku zote wamekua wakimuandika vibaya nahodha wake huyo. Huku akisema kwake yeye hajali kama Rooney anafunga ama hafungi, kikubwa ni kuisaidia timu ishinde.

Van Gaal anasema amefurahi kwa nahodha wake kufunga huku akisema inaweza kuwa chanzo cha mengi siku za usoni.



Comments