Rooney anavyochangia kuidhoofisha Man United


Rooney anavyochangia kuidhoofisha Man United

Katika mchezo wa Manchester Derby wikiendi iliyopita, kuna wakati ndani ya kipindi cha kwanza mshambuliaji na nahodha wa Manchester United alipata mpira akiwa upande wa kushoto wa lango la City na akaanza kuelekea kwenye eneo la penati la wapinzani wao. Muda huo huo, Anthony Martial akiwa kwenye nafasi nzuri – akijiandaa kutumia makosa ya Bacary Sagna ambaye alikuwa nje ya nafasi yake ili kwenda kumkaba Rooney. Rooney alipaswa kuona nafasi aliyokuwepo Martial na kumpa pasi mapema ndani ya Box lakini badala yake akachelewesha kutoa pasi na United ikapoteza nafasi nzuri ya kupata goli.

  Baadae kidogo mbeleni mwa mchezo – United walimpasi mpira mrefu Maroune Fellaini ili kutumia nguvu zake kuwavuta walinzi wengi wa City lakini ili mbinu hiyo ifanikiwe alikuwa anahitaji mchezaji wa kucheza pembeni yake ambaye angeweza kumpasia baada ya kuwavuta mabeki wa City – mchezaji huyo alikuwa Wayne Rooney – hata hivyo nahodha huyo wa United alikuwa anakwenda mbele kwa nadra sana – mara kadhaa alikuwa nyuma ya lango la City kwa yadi 30.

Kama kuna mechi ilitoa picha halisi ya namna kiwango cha Rooney kilivyoshuka basi ni mechi dhidi ya City. Ulikuwa ni mchezo ambao angependa kuusahau, Rooney alipiga shuti moja tu langoni – hakutoa pasi ya maana hata moja, hakufanya dribble hata moja na alimaliza mechi akiwa idadi ndogo zaidi ya pasi kwa wachezaji wote wa ndani siku hiyo.

 
Ujio wa Martial siku ya mwisho ya usajili ilibidi umuamshe Rooney na kukuza kiwango chake lakini badala yake ndio amezidi kuporomoka. Pamoja na Martial kuanza vyema lakini imebidi apelekwe upande wa kushoto ili kumpa nafasi Rooney kucheza kati. Wakati hili likimruhusu Herrera kucheza nyuma ya mshambuliaji, lakini linazorotesha mashambulizi ya United ambayo yanaongoza na Rooney. Kati mara zote 478 ambazo Rooney amegusa mpira msimu huu, ni mara 33 tu aligusa mipira hiyo kwenye eneo la penati la timu pinzani, rekodi mbovu kwa mshambuliaji wa kati.

Hata hivyo, pamoja na Rooney alivyo na kiwango kibovu, bado Louis van Gaal amegoma kumuondoa mshambuliaji huyo katika kikosi cha kwanza. Amekuwa akimtetea sana Rooney dhidi ya wachambuzi na waandishi wa habari wa michezo ambao wamekuwa wakimponda mara kwa mara. Inawezekana boss wa United alijichanganya mwenyewe kwa kumpa kitambaa cha unahodha Rooney – kitambaa ambacho kimempa Rooney ulinzi wa kutopigwa benchi – pamoja na kuwa katika kiwango kibovu msimu huu.

Takwimu zake za msimu huu ni mbovu kuliko zozote katika miaka 7 iliyopita. Haikupaswa kuwa hivi kwa Rooney – ukizingati kuondoka kwa Robin van Persie na Falcao – Rooney alipewa majukumu ya kuongoz mashambulizi ya United kwa mara nyingine tena, baada ya kucheza kwenye kiungo msimu uliopita. Ilikuwa ni nafasi nyingine ya Rooney kujiwekea himaya kama mshambuliaji tegemezi kama ilivyokuwa maimu wa 2009/10 na 2011/12, ambapo alifunga jumla ya magoli 53 ya ligi tu. Hata hivyo mpaka sasa katika mechi 9 amefunga magoli mawili tu.

 

Kwa mchezaji ambaye amerudishwa kwenye nafasi yake halisi, Rooney hafanyi jitihada za kurudisha ukali wake mbele la lango la adui. Wastani wa mashuti 2.1 kwa mchezo ni ndogo zaidi katika misimu yake 7 iliyopita ya EPL, pia anafeli kuwachezesha wengine akiwa na wastani 1.1 key passes kwa mechi – takwimu nyingine mbaya zaidi kwenye maisha yake ya soka. Pia wastani wa pasi 39.7 kwa mechi inamfanya awe mshambuliaji mwenye takwimu mbaya zaidi ya pasi katika Ligi kuu ya England.

  Bila kufunga magoli na kuwachezesha wenzie – Rooney amekuwa na mchango mdogo mno kwa United. Kuendelea kwako kuwemi kikosini kunadhoofisha maendeleo ya Martial na Depay – Martial akichezeshwa pembeni na Depay akibaki benchi. Jambo pekee zuri la kucheza kwa Rooney namba 9 ni Herrera kuchezeahwa nyuma yake, lakini ingekuwa bora zaidi kama Hererra angekuwa anacheza na nyuma ya MartiL – na sio Rooney ambaye kiwango chake kimeporomoka.

Moja ya mechi ambayo United walicheza vizuri sana msimu huu – ilikuwa kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya Liverpool – walishinda 3-1. Mechi hii Rooney hakucheza.
Japokuwa amekuwa akimtetea sana hadharani, kwa hakika nyuma ya pazia atakuwa anajiuliza aendelee kumpanga au amtose nahodha wake. Kwa kujaji kupitia kiwango ha msimu huu, ni suLa la muda tu kabla uvumilivu wa Mdachi haujaisha na kuamua kumuacha benchi nahodha wake.



Comments