Mwenyekiti wa Liverpool, Tom Werner amesema kuwa kama klabu walimpa muda wa kujitetea aliyekua kocha wao Brendan Rodgers kabla ya kumtimua wiki iliyopita.
Liverpool imempa mkataba kocha mjerumani, Jurgen Klopp mkataba mnono wa miaka 3 na mshahara wa pauni milioni 6 kwa msimu.
Rodgers alifukuzwa baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton huku Liverpool ikishika nafasi ya kumi na kukusanya points 12 katika michezo 8 waliyocheza msimu huu.
Mwenyekiti wa Liverpool, Tom Werner anasema, "wakati tunaingia mkataba na Rodgers, tulidhani tumepata kocha bora, lakini kwa Klopp tunaamini ni bora zaidi".
Mwenyekiti huyo anasema wanatakiwa kuwa 'optimistic' kwa ujio wa Klopp na kwamba wanaamini ataleta kitu tofauti klabuni hapo.
Comments
Post a Comment