ROBIN VAN PERSIE NA MEMPHIS DEPAY WAZINGUANA MAZOEZI ...KOCHA WA HOLLAND ANENA, VAN PERSIE ASUGUA BENCHI



ROBIN VAN PERSIE NA MEMPHIS DEPAY WAZINGUANA MAZOEZI ...KOCHA WA HOLLAND ANENA, VAN PERSIE ASUGUA BENCHI
Kocha wa Holland Danny Blind amekiri kuwa Robin van Persie na Memphis Depay walitibuana mazoezini kuelekea mchezo wao wa ushindi dhidi Kazakhstan siku ya Jumamosi.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kufa na kupona kwa Holland ambao ushindi ulihitajika kwa hali yoyote ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu Euro 2016.

Katika mchezo huo, Van Persie aliachwa benchi lakini Blind alisema hatua hiyo haikuwa na uhusiano wowote na ugomvi wa mshambuliaji huyo na Memphis Depay.

Blind akafafanua kuwa alimwacha benchi mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na Arsenal kwa kuamini kuwa bado hayuko fiti kisawasawa.
Robin van Persie (centre) was involved in a                  disagreement with Memphis Depay during training last                  week
Robin van Persie (katikati) alizinguana na Memphis Depay mwishoni mwa wiki iliyopita




Comments