Jumamosi ya jana klabu bingwa ya Ujerumani FC Bayern Munich iliendeleza ubabe wake katika Bundesliga baada ya kuiadhibu Werder Bremen na kuweka rekodi mpya kwenye ligi.
Goli pekee la Thomas Muller ilitosha kuipa Bayern rekodi mpya ya Bundesliga mwanzo mzuri zaidi wa timu kwenye ligi hiyo.
Vijana wa Pep Guardiola jana waliivunja rekodi yao wenyewe ya mwanzo mzuri wa ligi waliyoiweka msimu wa wa 2012/13.
Kwa ushindi wa jana sasa Bayern wanakuwa wameshinda mechi 9 mfululizo katika ligi hiyo, rekodi mpya kwenye Bundesliga.
Mabingwa hao wa Ujerumani sasa wana pointi 7 mbele ya Dortmund wanaoshika nafasi ya pili, na jumanne ijayo wanakutana na vijana wa Arsene Wenger katika mchezo wa 3 wa hatua ya makundi katika Champions League.
Comments
Post a Comment